KAZI YANGU

                                                         MAISHA YA KAWAIDA
Namshukuru mungu ambaye amenipa karama na vipawa mbalimbali katika maisha yakila siku
Achilia mbali mambo ya huma yangu ya kidini. Mimi ni mwalimu wa kiingereza,computer na masomo ya historia katika shule za sekondari.pamoja na kazi hizo pia Mungu amenijaalia utaalamu wa mziki kwa ujumla wake amabapo kwa sasa ninamiliki studio za kurekodi nyimbo ijulikanayo kwa jina la ZEZIKA RECORDS AND PRODUCTION iliyopo mtaa wa Kagera jijini mbeya.

MAISHA YA KIHUDUMA.
 Namshukuru mungu pia kwa kunijalia huduma mbalimbali za kiroho katika kuujenga mwili wa kristo.
Mpaka sasa ninatumika kataka huduma zifuatazo,
  1. Ni kiogozi wa huduma ya sifa na kuabudu katika kanisa la EAGT GILGAL MWANJELWA,
  2. Ni mwalimu mkuu wa kwaya ya PARAPANDA VOICE CHOIR ;
  3. Ni kiongozi wa ibada za kiingereza katika kanisa EAGT GILGAL MWANJELWA,
  4. Ni mkurugenzi wa huduma ya THE PARAPANDA OUTREACH MINISTRY, ambayo hujishughulisha na   kupeleka neno la mungu sehemu mbalimbali hasa ambazo hazijafikiwa pia huduma hii hujishughulisha na kuzisaidia jamii ambazo ziko katika mazingira magumu mfano wajane ,yatima na wazee mahitaji yao ya kila siku kama chakula, mavazi na elimu
  5. Pia nimwalimu wa neno la Mungu katika semina na makongamano mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni